Register Today And Join Thouthands Of Buyers , Sellers And Advertisers In Tanzania !   For FREE !

JINSI YA KUTENGENEZA UNGA WA LISHE

UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE. Mahindi ni miongoni mwa mazao ya chakula ambayo unga wake unatumika kutengeneza unga lishe. UNGA LISHE : Ni unga bora na unao hitajika sana katika kuborehs afya za watoto, wazee na wagonjwa. Ukiwa kama mjasiriamali mdogo, ni muhimu kujua namna ya kutengeneza unga lishe, kwani malighafi zinazo tumika katika utayarishaji wa unga huu zinapatikana kwa wingi na kwa bei nafuu, hivyo basi hata kwa wewe mwenye mtaji mdogo, unaweza kufanya biashara hii bila ya kuhitajika kuwa na mtaji mkubwa jambo linalo chukuliwa kama changamoto kwa wajasiriamali wengi nchini. MALIGHAFI ZINAZO HITAJIKA KATIKA UTENGENEZAJI WA UNGA LISHE. * Karanga - Nusu Kilo. * Soya - Nusu Kilo. * Ulezi - Kilo moja na Nusu. * Mahindi -Nusu Kilo *Mtama - Mtama Nusu Kilo. * Uwele - Nusu kilo. * Mchele - Nusu kilo.. JINSI YA KUTENGENEZA UNGA LISHE. 1. Safisha ulezi na kuutoa michanga pamoja na vumbi. 2. Kaanga soya kwenye moto mpaka ibadilike rangi na kuwa " brown " ama kahawia. 3. Kaanga karanga zako na toa maganda. Saga mchanganyiko wa malighafi zote hapo juu kwa pamoja, kisha anika juani mpaka ukauke, halafu weka kwenye vifungashio kwa ajili ya kuuza.

Back to top